Mezani Asubuhi; Neymar aaga Barcelona # PSG wamtaka Sanchez # Chelsea waigomea Man U # Mbappe huyoo Madrid
BARCELONA- MSHAMBULIAJI
mahiri wa Barcelona na Brazil, Neymar (25) amewaambia wachezaji wenzake kwamba,
anakwenda kujiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa. Hata hivyo, kocha wa Barcelona,
Ernesto Valverde amesema taarifa hizo ni tetesi kwani mchezaji huyo haondoki.
Le Parisien.
Matajiri wa Ufaransa, PSG, wametangaza kuwa wako
tayari kutoa dau la pauni milioni 70 (sh bilioni 203) kwa Arsenal, kwa ajili ya
kumsajili Alexis Sanchez. Pia PSG imesema itatoa mshahara wa pauni 400,000 (sh
bilioni 1.16) kwa mchezaji huyo aliyeonekana kwenye hoteli moja jijini Paris
kwa mazungumzo na timu hiyo. Mirror.
Dau la pauni milioni 35 (sh bilioni 101.5) la
Manchester United, kwa ajili ya kumsajili kiungo Nemanja Matic, limekataliwa na
Chelsea. Chelsea inadai kuwa, Matic anauzwa kwa pauni milioni 50 (sh bilioni
145). Mirror.
Monaco imekubali dau la pauni milioni 120 (sh
bilioni 348) kutoka Real Madrid, ili kumsajili mshambuliaji kinda, Kylian
Mbappe (18). Dau hilo linatarajiwa kuweka rekodi kwa sasa. Sun.
Barcelona imetoa onyo kwa kiungo mshambuliaji wa
Liverpool, Philippe Coutinho, kwamba itaachana na mpango wa kumsajili na
kumgeukia Ousmane Dembele wa Borussia Dortmund, endapo Liverpool watakataa dau
lao. Barcelona walitoa pauni milioni 70 (sh bilioni 203). Sun.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, amepnga kumsajili mshambuliaji
wa Swansea, Fernando Llorente (32), anayeuzwa kwa dau la pauni milioni 30 (sh
bilioni 87) ili asaidiane na Alvaro Morata. Pia, Chelsea wanamtaka winga wa
Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain. Sky Sports.
Dau
la Swansea City la pauni milioni 20 (sh bilioni 58), kwa ajili ya kumsajili kiungo
wa Arsenal, Jack Wilshere, limekataliwa. Telegraph.
No comments