Header Ads

Makamu wa Rais Nigeria amtembelea Buhari London




Muhammadu Buhari na makamu Rais Yemi Osinbajo Abuja Machi 13,2017
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, akisalimiana na Makamu wake, Yemi Osinbanjo katika moja ya mikutano yao Ikulu ya Nigeria kabla ya kiongozi huyo kuja London kwa matibabu.

LONDON- RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na kiongozi anayekaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Msemaji wa Kaimu Rais, Yemi Osinbanjo, alisema mkutano huo ulikuwa mzuri lakini hakutoa maelezo zaidi. Buhari amekuwa jijini hapa tangu Mei, akipata matibabu kwa ugonjwa ambao haujatajwa.
Osinbajo anategemewa kurudi Nigeria baada ya mkutano huo. Ukimya wake umeibua mjadala nchini humo, iwapo Buhari ataweza kurudi na kuendelea na majukumu yake ama la.

No comments

Powered by Blogger.