Lukaku asajiliwa Man United kwa pauni milioni 75

LIVERPOOL- Manchester
United imekubaliana na Everton dau la pauni milioni 75 (sh bilioni 217.5) kama
ada ya uhamisho ya mshambuliaji Romelu Lukaku ambaye kwa msimu uliopita
alifunga magoli 25.
Hayo yanajiri
muda mfupi, baada ya klabu hiyo ya Manchester kutangaza kuwa iko tayari
kuingilia kati usajili huo. Usajili huo huenda ukaathiri kwa kiasi kikubwa
usajili mwingine wa staa wa Real Madrid, Alvaro Morata.
United inatarajiwa
kukamilisha kila kitu kabla ya kuanza ziara yao ya Marekani, mapema wiki ijayo.
BBC Sport
No comments