Jioni Njema; No ofa kwa Aubameyang # Chelsea yamgeukia Danilo # Prince wa Monaco asema Mbappe haondoki # Dier hauzwi

BERLIN- BORUSSIA Dortmund imesema
hakuna ofa yoyote iliyowasilishwa mezani mwa klabu hiyo, ikiwa ni sehemu ya
usajili wa mshambuliaji wao, Pierre-Emerick Aubameyang.
Kauli hiyo
inakinzana na ile ya Chelsea ambao wamedai kutoa pauni milioni 70 (sh bilioni
203) ili kumpata mchezaji huyo. Pia, inadaiwa kuwa wakala wake amefanya
mazungumzo na PSG ya Ufaransa na AC Milan ya Italia.
Chelsea
imedaiwa kufanya mazungumzo na Real Madrid, kwa ajili ya kumsajili mlinzi wao
wa kulia, Danilo, ambaye anatakiwa na Juventus pia.
Sky Sports
imeelezwa kuwa, itawalazimu Chelsea kutoa pauni milioni 30 (sh bilioni 87) kwa
ajili ya kuipata huduma ya beki huyo.
Mwanamfalme
Prince II wa Monaco, anaamini kuwa staa wa timu ya Monaco, Kylian Mbappe
atabakia klabuni hapo na kusaini mkataba mpya.
Alipoulizwa kama
Mbappe anaweza akaondoka msimu huu, mwanamfalme huyo alisema; “Sidhani kama
hilo litatokea. Kuna mazungumzo yanaendelea na yananipa uhakika kuwa atabaki.”

Sky Sports
imeelezwa kwamba, Eric Dier hauzwi nab ado Tottenhma Hotspurs haijapokea ofa
yoyote inayomhusu kiungo huyo. Licha ya kuwepo kwa madai kuwa Man United
inamhitaji kwa udi na uvumba, vyanzo hivyo vinadai kuwa klabu hiyo inapoteza
muda wake.
Man United
imeongeza nguvu kwenye dili la uhamisho la winga wa Inter Milan ya Italia, Ivan
Perisic, ili kukamilisha usajili huo kabla ya wiki ijayo lakini Inter wamekaza
kuwa bei yake ni pauni milioni 48 (sh bilioni 139.2).
Atletico
Madrid wametangaza kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Sevilla,
Vitolo kwa mkataba wa miaka 5. Hata hivyo, mchezaji huyo ataenda kucheza kwa
mkopo Las Palmas hadi Januari mwakani kutokana na timu hiyo kuzuiwa na FIFA.

Klabu ya PSG inatarajiwa kumtangaza muda wowote
Dani Alves kuwa mchezaji wao, baada ya kukamilisha usajili wake mapema leo na
tayari ameshatua Paris.
No comments