Jeshi la Kenya lawasaka Al Shabaab msitu wa Boni Kenya
LAMU- JESHI la Ulinzi Kenya (KDF), limetuma vikosi
kadhaa vya wanajeshi wake, katika msiu wa Boni mjini hapa ili kuwasaka wanamgambo
wa Al Shabaab ambao jana walijaribu kuteka kituo cha polisi cha Pandaguo.
Hata hivyo, inatarajiwa kuwa KDF itapata wakati
mgumu kutekeleza zoezi lao wa kuwasaka na kuwabaini wanamgambo hao, kwani
wenyeji wa eneo hilo wamekuwa kimya bila kuoa taarifa zozote licha ya
wapiganaji hao kudaiwa kuswali katika moja ya misikiti ya hapo kabla ya
kushambulia kituo.
Inadaiwa kuwa, wanamgambo hao walifika msikitini
hapo majira ya saa 11 asubuhi na kuswali swala ya asubuhi msikitini hapo kabla
ya kuanza kuelekea kwenye utekelezaji wa unyang’anyi wao.
Baada ya kutoka msikitini hapo, wanamgambo hao
walielekea kituo cha polisi cha Pandaguo na wengine kwenye zahanati iliyo
karibu na kupora dawa na silaha kisha kutokomea.
Wanakijiji wameeleza kuwa walisikia milipuko kadhaa
nyakati za asubuhi leo, wakati KDF wakiendelea kutekeleza zoezi lao la kuwasaka
wanamgambo hao ambao wanadaiwa kufikia 150 walivamia kituo na kukimbilia
msituni humo.
Standard Newspaper
No comments