Ajali ya ndege yaua watu 16 Marekani
Ajali
hiyo ilitokea katika kaunti ya LeFlore karibu kilometa 160 kusini mwa mji mkuu
wa jimbo hilo, Jackson. Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.
Hakuna
taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo. Kwa
mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi, ndege hiyo ilianguka katika shamba
moja na mabaki yake yakatapakaa eneo lote.
No comments