Simba waendelea kutoroka mbugani Afrika Kusini

MPUMALANGA- WALINZI wa mbuga ya Kruger, wanawattafuta simba
wanne wa kiume ambao wametoroka kwenye mbuga hiyo.
Simba hao
walitoroka mbugani hapo Jumapili, na mara ya mwisho walidaiwa kuonekana katika
kijiji cha Matsulu. Usimamizi wa mbuga hiyo sasa umewataka wenyeji kuchukua
tahadhari
Bado haijabainika
ni kwa namna gani wanyama hao, walifanikiwa kutoroka na kutoka nje ya mbuga hiyo
inayozungukwa na uzio mkubwa.
Mbuga ya
kitaifa ya Kruger ni moja ya mbuga kubwa zaidi barani Afrika ikiwa na ukubwa wa
kilomita 19.485 mraba.
Kisa hiki
kinatokea baada ya simba wengine watano kutoroka mbuga hiyo Mei, mwaka huu.
Wanne walipatikana lakini mmoja bado hajulikani aliko.
BBC
No comments