Watu wawili wadaiwa kuuawa Kibiti
KIBITI- WATU wawili
wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi
wilayani hapa usiku wa kuamkia leo (Jumatano).
Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na
mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo na kusema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu na ukaguzi.
Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi.
Chanzo: Mwananchi
No comments