Header Ads

Ujerumani yakataa kumwachia jasusi wa Uswisi



Germany refuses to release Swiss spying suspect
KARLSRUHE- MAHAKAMAya Juu mjini hapa, imetupilia mbali ombi la kumwachia raia mmoja wa Uswisi ambaye anashikiliwa kwa madai ya kufanya upelelezi nchini.

Mwanaume huyo ambaye ametambuliwa kama Daniel M (54), alikamatwa mnamo April mwaka huu hotelini mjini Frankfurt kwa madai ya kufanya upelelezi nchini tangu mwaka 2012.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ilieleza kuwa ombi la kumwachia jasusi huyo limekataliwa na ataendelea kushikiliwa.

Upande wa mawakili wa Serikali, uliieleza mahakama hiyo kuwa Daniel M. amekuwa akipokea maagizo ya msingi kutoka kwa Shirika la Ujasusi la Uswisi (FIS) lakini hayo yaliyosababisha akamatwe yalikuwa muhimu zaidi na yalikuwa kinyume na matakwa ya Serikali ya Ujerumani.

Inadaiwa kuwa jasusi huyo alipewa jukumu la kuwabaini wapelelezi watatu wa Idara ya Kodi ya Ujerumani, ambao walinunua CD zenye taarifa za watu wenye akaunti za benki za kigeni kwenye mataifa yenye misamaha ya kodi kama Uswisi.

Taarifa alizokusanya Daniel M. zinadaiwa kuisaidia Uswisi kufungua kesi dhidi ya wapelelezi hao, kwa kuvunja sheria za kibenki za Uswisi na kufanya ujasusi wa kiuchumi.

Mbali na hayo, mawakili hao wa Serikali waliieleza mahakama kwamba jasusi huyo wa Uswisi anadaiwa kupandikiza kifaa maalum cha kukusanya taarifa kwenye jengo la Wizara ya Fedha ya Ujerumani, madai ambayo mtuhumiwa aliyakanusha.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba mara baada ya kukamatwa kwa jasusi huyo, Ujerumani na Uswisi zilisaini haraka makubaliano ya kusitisha ujasusi baina yao.

The Local

No comments

Powered by Blogger.