Picha mbalimbali za maandalizi ya Messi kufunga ndoa leo

Mshambuliaji wa timu ya Barcelona, Lionel Messi akiwa na mpenzi wake,
Antonella Roccuzzo na watoto wao, Thiago (mkubwa) na Mateo (mdogo). Messi
anatarajiwa kumuoa Antonella leo huko Rosario nchini Argentina.

Sehemu ya hoteli ya Rosario Hotel City Center ambako Lionel Messi
anatarajiwa kufungia ndoa na mwenza wake, Antonella Roccuzzo, ambaye (Messi) alikutana
naye akiwa na miaka mitano. Hoteli hiyo ipo katika mji wa Rosario ambao ndiko
alikozaliwa staa huyo.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay na Barcelona, Luis Suarez
akiwasili mjini Rosario kwa ajili ya kuhudhuria harusi ya rafiki yake mkubwa,
Lionel Messi ambayo inatarajiwa kufanyika leo.
Mbali na Luis Suarez, staa mwingine ambaye aliambatana nao ni Neymar
kutoka Brazil. Hata hivyo, inadaiwa kuwa nguli huyo wa Barca hakumwalika kocha
wake wa zamani, Pep Guardiola na mfalme wa soka wa Argentina, Diego Maradona.
No comments