Mwanamke azirai baada ya kuvunja bangili ya milioni 96 China

YUNNAM- MWANAMKE
mmoja nchini, amejikuta akizirai akiwa kwenye duka la kuuza vito vya thamani
baada ya kuvunja kimakosa bangili ghali yenye thamani ya dola 44,000 (sh
milioni 96.8).
Mtalii huyo
kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka moja
lililo mkoani hapa, karibu na mpaka na Myanmar. Alipoambiwa thamani na bangili
hiyo, aliivua kwa haraka, lakini ikaanguka kimakosa na kuvunjika.
Hakuna
makubaliano yaliyoafikiwa kuhusu namna ambayo bangili hiyo itafidiwa. Wafanyakazi
wa duka walijaribu kumtuliza baada ya kisa hicho, lakini mara moja alianza
kutokwa na jasho na kisha akazirai.
Alipata
nafuu wakati wateja wangine ambao walikuja kumsaidia walipomfinya pua yake. Wafanyakazi
wa duka walimwambia alipe dola 25,000 ili kutatua suala hilo, lakini yeye
alidai kuwa alikuwa na dola 1,500 tu.
Polisi walishindwa
kushawishi pande zote kufikia makubaliano na suala hilo huenda likaelekea
mahakamani. Chama kimoja cha kuuza vito vya thamani kilisema kuwa bangili hiyo
ni ya thamani ya dola 26,000 (sh milioni 57.2).
No comments