Machinga wabuni mbinu mpya kuwaepuka askari wa jiji Nairobi
NAIROBI-
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo maarufu Machinga jijini hapa, wamebuni mbinu mpya
ambayo inawawezesha kuepuka kukamatwa na askari wa jiji, katika harakati zao za
kibiashara.
Mbinu
hiyo ambayo imebainika kuwa ni kuja na watoto wao na kujifanya walemavu,
imefanikiwa kuwaepusha na vipigo kutoka kwa askari wa jiji ambao wamekuwa
wakiwakamata na kuwapeleka korokoroni kutokana na kufanya biashara kwenye
sehemu zisizoruhusiwa.
Akizungumza
na gazeti la The Star Kenya, mmoja wa ‘wamachinga’ hao amesema kuwa mbinu kubwa
anayoitumia ni kuja na mtoto wake mchanga kwenye eneo ambalo anafanyia biashara
ili asisumbuliwe na askari hao.
“Sijakamatwa
kwa muda mrefu wala kuonewa na askari wa jiji, tangu nilipoanza kuja na mtoto
wangu wa miaka miwili kazini hapa. Wakija wakinikuta na mtoto mdogo, basi
wananiacha na kuondoka zao,” alisema Alice Mueni ambaye anafanya shughuli za
biashara katika eneo la EastMatt Supermarket kwenye mtaa wa Tom Mboya.
Machinga
mwingine ambaye alijitambulisha kama Michael Wambugu, alisema kwamba; “Hii ni
wilaya yetu hivyo tunatakiwa kuishi hapa hapa. Wanataka sisi tuende wapi? Tutakuwa
hapa muda wote la sivyo tutaanza kuiba.”
Hata
hivyo, mbinu zao bado hazifui dafu kutokana na wamachinga hao kulazimika kuanza
kazi nyakati za jioni ambazo zinakuwa hazina usumbufu wowote tofauti na mchana.
No comments