Korea Kaskazini yaituhumu Marekani
NEW YORK- KOREA Kaskazini imeituhumu Marekani kwamba,
imeweka masharti magumu yasiyo ya haki kwenye ofa yake ya kutaka kufanya
mazungumzo ya amani na taifa hilo.
Kupitia Balozi
wake UN, Kim in Ryong, Korea Kaskazini iliwasilisha malalamiko hayo kwenye Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu masharti hayo ya Marekani.
Balozi Ryong
alisema kwamba ni itakuwa ni ‘kosa kubwa la kimahesabu’ kwa mataifa au watu
kuamini kwamba vikwazo vipya vilivyowekwa hivi karibuni vitaweza kuiziuia Korea
Kaskazini kufanya majaribio ya makombora na silaha nyinginezo za kinyuklia.
“Vitendo
vyao visivyo na busara wala maana, vinaweza kwenda kinyume na wao
walivyotarajia kwani vikwazo vyao haviwezi kuizuia Korea Kaskazini kufanya
majaribio ya silaha zake,”
“Marekani
imekuwa ikisisitiza kuwepo kwa majadiliano hata sasa, lakini haileti maana
kufanya majadiliano hayo ikiwa kuna masharti yasiyo ya haki yaliyoambatanishwa
kwa ajili ya kutupa presha,” alisema Balozi Ryong kwenye mkutano maalum
uliongozwa na Bolivia.
Marekani
imekuwa ikisema kwamba, iko tayari kujadiliana na Korea Kaskazini lakini iwapo
itasitisha mipango yake ya kufanyia majaribio makombora yake ya masafa na
silaha za kinyuklia. Mwezi huu, baraza hilo la UN, liliweka vikwazo vipya 14
kwa taifa hilo ambalo limekuwa likikiuka maagizo ya Umoja wa Mataifa.
No comments