Header Ads

Israel yaishambulia Syria



Ni siku ya tatu mfululizo kwa mashambulizi haya
TEL AVIV- ISRAEL imeshambulia ngome ya majeshi ya Syria kwa siku ya tatu mfululizo, baada ya kombora la wanajeshi hao kuanguka kwa bahati mbaya katika eneo Golan linaloshikiliwa na Israel.

Katika kisa hicho cha jana, vikosi vya Israel vilifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya eneo lao.
Israel imetekeleza mashambulizi kadhaa ya angani mara kwa mara au kujibu mashambulizi wakati wa mzozo wa Syria, lakini imejitenga kuhusika moja kwa moja na mzozo huo.
Israel iliuteka mji wa Golan kutoka mikononi mwa Syria wakati wa mapigano ya mwaka 1967.

No comments

Powered by Blogger.