Helikopta iliyoshambulia mahakama Venezuela yapatikana

CARACAS- VIKOSI vya usalama nchini, vimefanikiwa
kuipata helikopta iliyotumiwa na ofisa muasi wa polisi kupaa juu ya majumba ya Serikali
mjini hapa na kushambulia jengo la Mahakama ya Juu kwa kuangusha guruneti na
kupiga risasi jana.
Makamu wa Rais, Tareck El Aissami amesema helikopta
hiyo ilipatikana karibu na karibu na jimbo la Vagas lililopo pwani ya Kaskazini
mwa nchi, kilometa 45 kutoka hapa Caracas.
Alitoa picha
zinazoonesha helikopta hiyo katika maeneo ya milima ikisafisha maeneo
yaliyozungukwa na migomba ya ndizi.
Kufikia sasa
hakuna dalili yoyote ya kupatikana kwa rubani wa helikopta hiyo, Oscar Lopez, ambaye
alikuwa ni ofisa polisi aliyeamua kuasi na kutekeleza kitendo kilichodaiwa na Serikali
kama kisa cha kigaidi.
No comments