Header Ads

Chanjo isiyo salama yaua watoto 15 Sudan Kusini



Watoto wa Sudan kusini
JUBA, Sudan Kusini
SERIKALI imesema watoto wapatao 15 wamekufa, ikiwa ni matokeo ya makosa yaliyofanyika katika jaribio la kuwakinga na ugonjwa wa surua.

Wafanyakazi wa afya katika jimbo la Ikweta Mashariki, walirudia tena kutumia sindano zisizo safi kuwachanja watoto wote.
Waziri wa Afya nchini, Riek Gai Kok alisema timu iliyohusika katika kampeni hiyo ya chanjo haikuwa na vigezo wala kupata mafunzo kwa kazi hiyo.
Huduma za afya zimekuwa zikifanya kazi kwa shida nchini, tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 2013.

No comments

Powered by Blogger.