Zitto apokea barua ya kujiuzulu ya wakili Albert Msando
Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba
kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando anawajibika kwani anapaswa, nanukuu
kutoka katika barua yake, “kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka”.
Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango
mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama
kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni
matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri
atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika
kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa
uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
No comments