Korea Kusini washambulia kifaa cha Korea Kaskazini
Sehemu ya mpakani mwa Korea Kusini na Korea Kaskazini linalojulikana kwa jina la Paju. Eneo hilo hakuna shughuli za kijeshi zinazoruhusiwa kufanyika.
SEOUL, Korea Kusini
SERIKALI imesema
kuwa imekishambulia ‘kifaa’ kutoka Korea Kaskazini kilichorushwa katika eneo maalum
lisilo la kijeshi.
Takriban
risasi 90 zilifyatuliwa zikielekezwa kwa kifaa hicho, ambacho kufikia sasa
hakijajulikana kilikuwa ni nini hasa. Miaka iliyopita, Korea Kaskazini ilirusha
ndege zisizokuwa na rubani katika mpaka huo.
Katika
taarifa yao, jeshi la Korea Kusini limesema kuwa limeweka ulinzi mkali. Kisa
hicho kinajiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika rasi ya Korea. Siku ya
Jumapili Pyongyang, ilitekeleza kile ilichodai kuwa jaribio lililofanikiwa la
kombora la masafa ya kadri.
Jaribio hilo
linajiri wiki moja baada ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio kile ilichodai
kuwa ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia, ambalo lina uwezo
wa kushambulia Marekani.
Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa, lilitarajiwa kufanya kikao cha faragha kuhusu
Korea Kaskzini jana jioni. Katika taarifa siku ya Jumatatu, lilikubali kuchukua
hatua muhimu ikiwemo vikwazo ili kuishinikiza Korea Kaskazni kusitisha hatua
yake.
Ongezeko
hilo la wasiwasi linajiri wakati ambapo kuna rais mpya nchini, Moon Jae ambaye
alikula kiapo cha kuchukua mamlaka mapema mwezi huu baada ya mtangulizi wake Park
Geun Hye kushtakiwa.
No comments