Wasamaria
wema na maofisa wa usalama wakiendelea na zoezi la kufukua vifusi kutafuta watu
waliokwama, baada ya ukuta kuanguka na kuua zaidi ya watu 22.
|
|
RAJASTHAN, India
TAKRIBAN watu 22 wamefariki baada ya ukuta
kuwaangukia wakati wa harusi kaskazini mwa India.
Wageni hao walikuwa wamejikinga na mvua kubwa
inayoendelea kunyesha kabla ya ukuta huo kuwaangukia.
Watu wengine
26 walijeruhiwa katika jali hiyo ya Bharatpur, wilaya moja ya jimbo la
Rajasthan, 15 kati yao wakiwa na majeraha mabaya.
Vyombo vya habari vinasema kuwa vibanda vya kuuza
chakula vilikuwa vimewekwa kandakando ya ukuta huo karibu na harusi.
Ukuta huo na kibanda ulianguka kutokana na kimbunga
kulingana na afisa wa Polisi Anil Tank aliyenukuliwa akisema.
Alisema kwamba ukuta huo wenye urefu wa futi 90
uliwaangukia wageni wengi.
''Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali za
eneo hilo mara moja huku wakipewa matibabu''.
|
No comments