|
MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesema
kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangazia zaidi ubingwa wa ligi ndogo
ya klabu Ulaya, Europa League.
Mourinho (pichani),
ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo badala ya kumaliza katika nafasi nne za
kwanza Ligi ya Premia, anasema uamuzi wake ni wa busara.
United wanaongoza 1-0 dhidi ya Celta Vigo
nusufainali kutoka kwa mechi ya kwanza wanapoelekea kwa mechi ya marudiano leo
Alhamisi jioni uwanjani Old Trafford.
Mourinho amesema kuwepo kwa mechi nyingi ambazo
klabu yake inahitajika kucheza kumemlazimu kuamua ataangazia wapi.
“Kucheza mechi kumi na saba katika wiki saba
haiwezekani. Si kamari, ni matokeo tu ya hali ilivyo. Ulikua uamuzi rahisi sana
kuufanya, uamuzi wa busara,” alisema Mourinho.
Mabingwa wa Europa League huhakikishiwa nafasi
katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, sawa na klabu zinazomaliza naafsi nne za
kwanza Ligi ya Premia.
Manchester United walishuka hadi nafasi ya sita
Jumatano baada ya Arsenal kuwalaza Southampton 2-0 Jumatano.
Arsenal waliwalaza United Jumapili katika mechi
ambayo Mourinho aliwapumzisha wachezaji wengi wake nyota kwa ajili ya mechi ya
Alhamisi.
Mourinho anaamini kwamba kushinda Europa League
ndio njia nzuri zaidi iliyosalia ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
|
|
 |
|
Wayne
Rooney amefunga mabao saba mechi 38 msimu huu
|
Amesema hatakuwa na majuto kamwe iwapo watashindwa
kutwaa ubingwa."Hebu tusubiri tuone kama tutaweza," alisema.
"Haijalishi nini kitatokea. Hakuna majuto,
tutajitolea kadiri ya uwezo wetu, mimi na wachezaji."
Mshambuliaji wa United Wayne Rooney anaunga mkono
msimamo wa Mourinho.
"Kusema kweli, ni vigumu kufuzu kwa kupitia
ligi. Tunaweza tukaangazia kushinda kikombe." (BBC)
No comments