Trump atakiwa kusalimisha kanda za mazungumzo yake na Comey
Kiongozi
wa Democrats katika bunge la seneti, Charles Schumer alionya kuwa uharibifu wa
kanda hizo utakuwa uvunjaji wa sheria.
Naye
Seneta wa Republican Lindset Graham alisema kuwa Ikulu ya Whitehouse inahitaji
kuwa wazi kuhusu iwapo kulikuwa na kanda zozote za rekodi za mazungumzo hayo au
la.
Mwito
huo unajiri baada ya Rais Trump kuandika maneno katika mtandao wake wa Twitter,
yanayoonekana kuwa vitisho kwa mkuu huyo wa zamani wa FBI.
Alimuonya
Comey wiki iliopita dhidi ya kuzungumza na vyombo vya habari, akisema anatumai
hakuna rekodi za mazungumzo yao. Ikulu ya Whitehouse haijathibitisha wala
kukana kuwepo kwa kanda hizo.
Schumer
pia alionya kwamba masenata wa chama cha Democrats, watakataa kumuunga
mkurugenzi mpya wa FBI hadi pale mtaalam atakapochaguliwa kuchunguza hatua ya
Urusi kuingilia masuala ya Marekani katika uchaguzi uliopita.
FBI
inachunguza madai hayo pamoja na ushirikiano wa Urusi na kampeni ya Rais Trump,
licha ya kiongozi huyo kukanusha mara kwa mara kuhusu uhusiano wowote na
aliongeza kuwa hakuna uhusiano wowote baina ya Comey kufutwa kazi na uchunguzi
huo.
Anasema
kuwa alimpiga kalamu Comey kwa sababu alikuwa ameshindwa kufanya kazi vizuri. Wanachama wa Democrats wamemshutumu Trump kwa
kumfuta kazi Comey ili kujaribu kusitisha uchunguzi wa FBI.
BBC
No comments