‘Trump aliitaka FBI kusitisha uchunguzi dhidi ya Flynn’
WASHINGTON
DC, Marekani
RAIS Donald
Trump alimtaka aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la FBI James Comey kusitisha
uchunguzi uliokuwa ukiendelea dhidi ya aliyekuwa mshauri wa masUala ya usalama,
Michael Flynn.
Kulingana na
barua iliyoandikwa na James Comey, Trump alimwambia kiongozi huyo wa FBI
kwamba; “Natumai utawachana na haya,” katika mkutano uliofanyika Ikulu ya
Whitehouse mnamo Februari mwaka huu.
Barua hiyo
iliandikwa mara moja baada ya mkutano, siku moja baada ya Michael Flynn
kujiuzulu kulingana na vyombo vya habari vya Marekani. Ikulu ya Whitehouse
imekana ripoti hiyo kwa taarifa.
“Rais Trump
hajamtaka Comey ama mtu yeyote kusitisha uchunguzi ikiwemo uchunguzi wowote
unaohusiana na jenerali Flynn,” ilisema.
Flynn
alilazimika kujiuzulu Februari mwaka huu, baada ya kumdanganya makamu wa rais
kuhusu mazungumzo yake na Balozi wa Urusi kabla ya Trump kuchukua mamlaka.
Mgogoro huo
wa hivi karibuni kuhusu Urusi, ulioripotiwa mara ya kwanza na gazeti la The New
York Times, unajiri wiki moja baada ya Trump kumfuta kazi Comey kuhusu
alivyofanya uchunguzi wa matumizi ya barua pepe za kibinafsi uliotekelezwa na
Hillary Clinton akiwa waziri.
Kufutwa kazi
kwa Comey kulizua hisia kali nchini, huku wakosoaji wakimshutumu Rais Trump kwa
kujaribu kusitisha uchunguzi huo wa FBI kuhusu madai kwamba Urusi iliingilia
uchaguzi wa Marekani mbali na ushirikiano wa maofisa wa Trump na Urusi.
No comments