Msichana amkata uume kiongozi wa dini India
KERALA, India
MSICHANA
mmoja wa umri wa miaka 23 nchini, amekata uume wa kiongozi mmoja wa dini jimboni
hapa kwa madai kwamba mwanaume huyo amekuwa akimbaka kwa miaka kadhaa.
Polisi wamesema
kuwa kiongozi huyo wa dini aitwaye, Gangeshananda Theerthapada, alikuwa akienda
kwenye nyumba ya mwanamke huyo kufanya maombi kwa ajili ya afya ya baba wa
mwanamke huyo.
Hatua ya
kiongozi huyo wa kidini kwenda nyumbani kwa msichana huyo, ilikuja baada ya
mama yake kuwa na matumaini kuwa mtu huyo ya Mungu angetatua matatizo ya
familia yake. Badala yake binti yake alidai kuwa alimdhulumu kingono kila mara.
Tukio hilo
lilitokea Ijumaa usiku, mara baada ya kiongozi huyo kufika hapo na kuanza
shughuli yake kisha kuelekea kumbaka msichana huyo ambaye alichukua kisu na
kumshambulia na kisha kuwaita polisi mwenyewe.
Mtuhumiwa
huyo wa ubakaji, alikimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura. Hospitali
hiyo ilisema mwanamume huyo wa miaka 54 kutoka Kollam alilazwa kwenye hospitali
hiyo.
Hata hivyo,
madaktari walieleza kuwa uume wa kiongozi huyo wa kidini ulikuwa umekatwa kwa
asilimia 90 na hakuna uwezekano wa kurudishwa tena. Madaktari walijaribu kuzuia
kufuja kwa damu na kumfanyia upasuaji ili aweze kupitisha mkojo.
No comments