Header Ads

Mchungaji aliwa na mamba akimwigiza Yesu

HARARE, Zimbabwe
MCHUNGAJI wa Kanisa la Saint of the Last Days, Jonathan Mthetwa ameshambuliwa na kuliwa na mamba watatu wakati akionesha jinsi Yesu alivyotembea juu ya maji.

Mthethwa juzi alihamishia maombi yake kwenye eneo hilo ambalo linajulikana kama Mto wa Mamba (Mto Mpumalanga), na kujaribu kuonesha kwa vitendo imani hiyo ya kibiblia.
Kwa mujbu wa mashuhuda, Mchungaji huyo aliingia majini na kujivuta umbali wa takriban meta 30 kabla ya kujaribu kutoka nchi kavu. Bahati mbaya kwa Mchungaji huyo, mamba watatu walimvamia na kumla.
Ni makubadhi na nguo yake ya ndani pekee ndivyo vilivyopatikana, kwa mujibu wa gazeti la The Daily Post la hapa.
Shuhuda Deacon Nkosi alisema: “Mchungaji alitufundisha kuhusu imani Jumapili iliyopiya. Aliahidi angetuonesha imani yake leo, lakini kwa bahati mbaya akaishia kufa maji na kuliwa na mamba wakubwa watatu mbele yetu.
“Bado hatuelewi kilichotokea, kwa sababu alifunga na kusali kwa wiki nzima. Walimmaliza kwa dakika chache kabisa. Kilichosalia walipomaliza kumla ni jozi ya makubadhi na nguo yake ya ndani ndivyo vilivyokuwa vikielea juu ya maji.”
Wakati waokoaji wakiwasili eneo la tukio, tayari Mchungaji alishaliwa.

 

No comments

Powered by Blogger.