Header Ads

Mahakama ya Katiba kuamua hatima ya Zuma



Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
PRETORIA, Afrika Kusini
MAHAKAMA ya Katiba nchini, inatarajiwa kuamua kuhusu iwapo wabunge wanaweza kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma, au la.

Hatua hiyo inajiri kufuatia hali ya sintofahamu kuhusu uongozi wa Zuma, huku kukiwa na madai ya uajiri wa marafiki zake Serikalini na ufisadi.
Zuma (pichani) hivi karibuni alizomewa katika baadhi ya mikutano ya hadhara huku maofisa wakuu wa chama chake wakionekana hadharini kujipigia debe ili kumrithi kiongozi huyo kama kiongozi wa chama.
Upinzani unadai kwamba wabunge wanastahili kuongozwa imani yao na sio uongozi wa vyama vyao, kwa kuwa uongozi wa rais Zuma ni suala muhimu la kitaifa.
Hatua hiyo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye ilisababishwa na kumfuta kazi Waziri wa Fedha, Pravin Gordhan na naibu wake miezi miwili iliopita. Hatua hiyo ilifanya uwezo wa kifedha wa taifa hilo kushuka.
Hata hivyo, baadhi ya wachunguzi wanaamini kwamba hata iwapo Mahakama ya Katiba itawapatia wabunge haki ya kupiga kura kwa siri, wanachama wengi wa ANC watamuunga mkono kiongozi.
Kama alivyosema mbunge mmoja, hataki kufuata wito wa upinzani na kwamba atakabili suala la Zuma kama la ndani ya chama.

No comments

Powered by Blogger.