Mchuuzi akiwauzia wapita njia na
wenye magari panya waliochomwa eneo la Salima, Malawi, Jumatatu wiki iliyopita.
Panya hao hupendwa na watu nchini humo na biashara yake hunoga hasa vijijini.
Mwendesha pikipiki wa mashindano
ya pikipiki wa Afrika Kusini akiwatumbuiza watu waliofika kwenye sherehe za
kuadhimisha miaka 50 ya kuwepo kwa jimbo la Lagos, nchini Nigeria.
Wakulima wakijitayarisha kuuza
mifugo wao kwenye maonesho katika soko kubwa zaidi la kilimo barani Afrika huko
Bothaville, Afrika Kusini yaliyofanyika wiki iliyopita.
Chanzo: BBC
No comments