Kupanda na kushuka kwa Profesa Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo
Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepitia misukosuko
katika nafasi za uwaziri tangu alipoteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya
Kikwete.
Leo Rais John Magufuli amemtaka Profesa Muhongo ajitathmini kuhusu
nafasi yake ya Uwaziri baada ya kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu.
Mei 2012, Rais Kikwete alimteua Muhongo kuwa mbunge pamoja na
wabunge wengine watatu, akiwamo Janet Mbene na James Mbatia. Baada ya kuteuliwa
na kuwa mbunge, Muhongo aliteuliwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini na
Rais Kikwete.
Hata hivyo Januari 24 mwaka 2015, alimuandikia Rais barua ya
kujiuzulu kutokana na sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta
Escrow.
Mwaka mmoja baadaye, baada ya Rais John Magufuli kuingia
madarakani, alimteua tena Profesa Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Muhongo
alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa tiketi ya CCM, katika
uchaguzi wa 2015.
Lakini leo tena, ikiwa ni miaka zaidi ya miwili tangu ajiuzulu
kutokana na kashfa ya Escrow, ametakiwa kujiuzulu kutokana na sakata la
mchanga wa madini.
Chanzo: Mwananchi
No comments