Header Ads

Bintiye Mugabe ateuliwa bodi ya udhibiti vyombo vya habari Zimbabwe



Bona Mugabe-Chikore
Bona Mugabe (katikati) akiwa na baba yake, Rais Robert Mugabe (kulia). 
HARARE, Zimbabwe
BINTI wa kipekee wa Rais, Robert Mugabe, Bona Mugabe-Chikore, ameteuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini, katika kile ambacho wakosoaji wanasema ni hatua ya kusaka taarifa zinazoipinga familia hiyo hususan katika mitandao ya kijamii.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Charity Charamba pia atahudumu katika bodi hiyo ya watu 11 iliyoteuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Ignatious Chombo, pamoja na wawakilishi wa makundi ya makanisa, wataalamu wa sheria na uhasibu na viongozi wa kitamaduni.
Shirika la kitaifa la habari limesema, bodi hiyo itadhibiti na kukagua vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini na kulenga ‘matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati pia ikizingatia uchaguzi mkuu unaowadia mwaka ujao’.
Bona amesoma nchini Singapore, na ana shahada ya uzamili katika masuala ya usimamizi, hususan wa mabenki na fedha.

No comments

Powered by Blogger.