Korea Kaskazini yadai Hwasong 2 linabeba kichwa cha nyuklia
Kombora
hilo lililorushwa katika mji wa Kusong, lilienda angani urefu wa kilomita 2,000
na kusafiri kilomita 700 kabla ya kuangukia baharini Magharibi mwa Japan.
Jeshi
la Korea Kusini limesema kuwa haliwezi kuthibitisha madai hayo ya Korea
Kaskazini. Lakini limesema kuwa kombora hilo lilionekana kuweza kuruka angani,
hatua ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa makombora ya masafa marefu
kulingana na kituo cha habari cha Yonhap.
Majaribio
ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo,
yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa (UN) na yamesababisha wasiwasi miongoni
mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.
Marekani
na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa mapema kesho.
Shirika
la habari nchini (KCNA), limesema kwamba jaribio la kombora jipya la masafa
marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa. KCNA ilieleza kuwa jaribio
hilo lililenga kuonesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa
cha nyuklia.
BBC
No comments