Kiongozi wa zamani FBI kuchunguza udukuzi wa Urusi
WASHINGTON
DC, Marekani
Wizara ya Sheria
nchini, imetangaza kuteuliwa kwa Mwendesha Mashtaka maalum atakae ongoza
uchuguzi wa tuhuma iwapo Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana.
Mwendesha
mashtaka huyo, Robert Mueller (pichani) aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijajusi la FBI. Pia
katika uchunguzi wake, atazingatia iwapo kulikuwa na mwingiliano wa aina yoyote
kati ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.
Taarifa
iliyotolewa na wizara hiyo, ilisema uchunguzi huo utaongozwa na mtu asiyeegemea
upande wowote kwa ajili ya maslahi ya umma.
Tangazo hilo
linafuatia utata uliojitokeza, kufuatia kufutwa kazi wiki moja iliyopita kwa
James Comey, ambae ndiye aliyekuwa akiongoza uchunguzi huo
No comments