Header Ads

Keown: Wenger wauze Sanchez na Ozil



Kwa pamoja Sanchez na Ozil wamekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Arsenal
LONDON, Uingereza
MLINZI wa zamani wa klabu ya Arsenal, Martin Keown amesema kuwa meneja wa Klabu hiyo, Arsene Wenger anapaswa kuwauza nyota wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil baada ya kuongeza muda wa kusalia kuinoa miamba hiyo ya London.

Mfaransa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na amesema kuwa, timu yake inaweza kupigana na kutwaa ubingwa msimu ujao. Viungo Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa pamoja wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa mwaka huu.
Keown alisema kuliko kupata hasara ya kuwaruhusu kuondoka bure, ni vema akafanya maamuzi magumu ya kuwauza nyota hao na kutengeneza faida itakayoweza kuleta wachezaji wapya na wenye morali kubwa zaidi.
Sanchez alifunga magoli 24 na kuchangia kupatikana kwa mengine 10, huku Ozil akifunga 8 na kuchangia 9 lakini yote hayo hayakutosha kuipa timu hiyo nafasi ya michuano ya mabingwa wa Ulaya msimu ujao, jambo ambalo linatia ukakasi kwa Sanchez na Ozil kuongeza mikataba yao.
Sanchez amepewa ofa ya paundi 300,000 kwa wiki lakini bado hajasaini mkataba huo, huku Ozil akikataa paundi 250,000 kwa wiki.


No comments

Powered by Blogger.