Header Ads

Aliyemuoa mwalimu wake aomba ndoa yao ivunjwe Marekani



https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/11B96/production/_96289527_c8825a2e-e3fc-48ad-91f2-1ac1bbb9c017.jpg
Wanadoa Mary Kay Fualaau (kushoto) na Vili Fualaau
WASHINGTON DC, Marekani
MWANAMUME mmoja ambaye hapo awali alizua mjadala mkali nchini, amewasilisha kesi mahakamani akitaka atengane na mkewe ambaye ni mwalimu wake wa zamani aliyefungwa kwa kufanya nae ngono akiwa na umri wa miaka 12.

Vili Fualaau, ambaye sasa ana umri wa miaka 33, aliwasilisha nyaraka za kesi kwenye Mahakama ya jimbo hili, akitaka ndoa yake ya miaka 12 na mkewe, Mary Kay Fualaau (zamani akijulikana kama Letourneau), mwenye umri wa miaka 55 ivunjwe.
Fualaau aliolewa akiwa na umri wa miaka 34 (akiwa na watoto wanne alipoanza uhusiano wa kindoa na Vili Fualaau) baada ya kutumikia kifungo cha miaka saba na miezi sita jela, wawili hao walioana kwa siri mnamo mwaka 2005.
Fualaau aliwasilisha kesi ya kuachana nae mapema mwezi huu, bila kuelezea sababu ya uamuzi wake huo. Katika ombi lake kwa mahakama, aliandika kwamba iwe yeye wala mkewe hakuna aliye na mali wala mkopo.
Aidha, Fualaau, ambaye ana watoto wawili na mkewe, alisema kwa sasa hawamtegemei tena, akiomba wawili hao wagawanyiwe kile kidogo walichoweza kutafuta pamoja kwa haki.
Hata hivyo, mkewe hajatoa kauli yoyote kwa umma juu ya uamuzi wa mumewe. Fualaau alikuwa darasa la sita alipoanza uhusiano wa kimapenzi mjini Seattle mwaka 1996.
Akiwa mwalimu, Fualaau alikamatwa mwaka 1997 alipokuwa na mimba ya mtoto wao wa kwanza, na baadaye alikiri kufanya kosa la ubakaji wa mtoto.
Hukumu yake ya kwanza ya miezi sita ilipunguzwa baadae na kuwa ya miezi mitatu, chini ya misingi kwamba angelikosa mawasiliano na mwanafunzi wake wa zamani. Lakini katika kipindi cha wiki kadhaa wawili hao walikamatwa wakifanya ngono, na akafungwa miaka saba.

No comments

Powered by Blogger.