Trump aionya tena Korea Kaskazini
Melivita
ya Marekani iitwayo
WASHINGTON DC, Marekani
RAIS Donald Trump kwa mara nyingine ameionya Korea
Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, kwa kusema kuwa taifa hilo linatafuta
matatizo.
Aidha, Trump alilitaka taifa la China ambalo ni
mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano
bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani
haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini pasipo uwepo wa China.
Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita,
lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa. Marekani imetuma meli za
kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea, hatua ambayo imechochea ghadhabu ya
Korea Kaskazini.
BBC
No comments