Header Ads

Mbeki awaunga mkono wapinzani wa Zuma



Thabo Mbeki
PRETORIA, Afrika Kusini
RAIS Mstaafu nchini, Thabo Mbeki amewataka wabunge wa chama cha ANC kutenda yatakayowafaa raia na sio kile kitakachofaidisha chama, wakati wa kujadili muswada wa kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma, wiki ijayo.
Mwito wa huo wa Mbeki (pichani), huenda ukawakera watu wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga muswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.

Upinzani unadai kuwa Zuma ni fisadi na kuwa alimfuta kazi Pravin Gordhan kama Waziri wa Fedha, licha ya kuwa Gordhan aliheshimika kwa kiasi kikubwa. Wanasema nia ya Zuma ilikuwa kuchukua usukani katika wizara ya fedha.
Zuma amekuwa akikanusha madai ya ufisadi, akisema kuwa yeye kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ni kwa manufaa ya raia
Kulingana na tovuti hiyo, Mbeki alisema kuwa wabunge wanafaa kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vya kisiasa. Anasema huu ni wakati wa Afrika Kusini kujua ukweli kuhusu uhusiano wa kikatiba kati ya wananchi na viongozi wao wa kisiasa.
Mbeki ni mwanachama wa ANC ambaye alijiuzulu kama rais baada ya kupoteza imani kwa chama hicho kinachoongozwa na Zuma, mwaka wa 2008.

No comments

Powered by Blogger.