Amnesty: China imenyonga watu wengi zaidi mwaka jana
Mwaka jana, idadi hiyo ilipungua kwa zaidi ya theluthi moja. Lakini Amnesty imesema kwamba, kiwango hicho hakihusishi China, ambayo inatuhumiwa kuwa na idadi kubwa ya adhabu ya kifo.
Inakadiriwa kwamba, idadi ya waliopata adhabu ya kifo nchini China mwaka jana, ni kubwa zaidi kuliko duniani kote.
Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja, Marekani haipo katika kundi la nchi tano zinazotumia adhabu ya kifo ambazo ni China, Iran, Saudi Arabia, Iraq na Pakistan.
Nchi ya Belarus na Mamlaka za Palestina zilirejesha adhabu ya kifo mwaka wa 2016. Botswana na Nigeria nazo zilitekeleza hukumu ya kwanza ya kifo mwaka wa 2013.
No comments