Header Ads

Zuma atakiwa kutohudhuria maziko ya mpinga ubaguzi




https://businesstech.co.za/news/wp-content/uploads/2015/12/Jacob-Zuma-in-Germany.jpg
CAPE TOWN, Afrika Kusini
RAIS Jacob Zuma hatahudhuria mazishi ya mwanaharakati wa kuipinga Serikali ya Ubaguzi wa Rangi, Ahmed Kathrada kwa ombi la familia yake.
Kathrada alimtaka Zuma (pichani) ajiuzulu mwaka uliopita, kufuatia kashfa za ufisadi na kuilazimu Serikali kuwakilishwa na Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa kwenye mazishi hayo.

Kathrada mwenye umri wa miaka 87, aliaga dunia jana. Aliwahi kufungwa pamoja na Mandela kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Alitumikia kifungo cha miaka 26 gerezani kabla ya kauchiliwa mwaka 1989. Baadaye alihudumu kama mshauri wa rais wa zamani Nelson Mandela, kwenye Serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia.
Zuma alikuwa ameagiza bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo chake, na kuahirisha mkutano wa mawaziri ili maofisa wapate kuhudhuria mazishi yake. Hata hivyo Zuma hatadhuria mazishi wala ibada ya maombi ambayo itafanyika baadaye wiki hii, kufuatia ombi la familia ya Kathrada.
Mke wa Kathrada, Barbara Hogan anafahamika kuwa mkosoaji mkubwa wa Zuma. Awali, Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu baada ya Mahakama ya Katiba nchini kuamua kuwa alikuwa amekiuka Katiba kwa kukataa kulipa fedha ambazo zilitumiwa kukarabati makao yake ya kibinafsi huko Nkandla.

 Ahmed Kathrada alifungwa miaka 26 jela

Mwanaharati mpinga ubaguzi uliokuwa ukifanywa na utawala wa kikaburu nchini Afrika Kusini, Ahmed Kathrada ambaye alifariki jana.




No comments

Powered by Blogger.