Sakata la kufoji cheti; Joho ahojiwa na polisi Mombasa
![https://3dwnh01icn0h133s00sokwo1-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2016/02/joho.jpg](https://3dwnh01icn0h133s00sokwo1-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2016/02/joho.jpg)
MOMBASA,
Kenya
GAVANA wa
jimbo la Mombasa nchini, Hassan Joho ameandikisha taarifa katika ofisi za
polisi wa kuchunguza jinai katika mji huo kuhusiana na tuhuma kwamba alighushi
cheti cha mtihani wa kidato cha nne.
Baraza la
Taifa la Mitihani Kenya (KNEC), linadai mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani
cha ODM, alighushi cheti cha mtokeo ya mtihani wa kidato cha nne kumuwezesha
kukubaliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi.
Joho (pichani),
ambaye ni naibu kiongozi wa chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani
Raila Odinga, amekanusha madai hayo na kudai kwamba Serikali imeibua tuhuma
hizo ili kumpiga vita.
“Nawaambia
kwamba, wanachofanya ni kujaribu kuwaaminisha kuwa sitakuwa kwenye karatasi za
wagombea urais lakini nawahakikishia kwamba mradi tu niwe hai, nitakuwa kwenye
kura wakati wa uchaguzi Agosti,” Joho aliwaambia wafuasi wake baada ya kuhojiwa
na polisi, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.
Barua ya
kaimu ofisa mkuu mtendaji wa baraza la mitihani (KNEC), M. G Karogo ambayo
ilitumwa kwa maofisa wakuu wa uchunguzi wa jinai inaonesha mwanafunzi kwa jina
la Ali Hassan alifanya mtihani wake katika shule ya upili ya 1993 na akapata
alama D- ambayo haiwezeshi mtu kujiunga na chuo kikuu.
Gavana huyo
anadaiwa kughushi cheti cha kuonesha alipata alama ya C+ katika mtihani wa
mwaka 1992 na akatumia cheti hicho kujiunga na chuo kikuu cha Nairobi ingawa
hakumaliza masomo yake.
Joho
alijiunga na Chuo Kikuu cha Kampala na akafuzu na shahada katika usimamizi wa
biashara mwaka 2013. Pia, ana shahada nyingine ya kwanza kutoka chuo kikuu cha
Gretsa cha Kenya.
Nchini
Kenya, gavana anahitajika kuwa na angalau shahada ya kwanza kutoka kwa chuo
kikuu kinachotambulika nchini ndipo akubaliwe kuwania wadhifa huo. Jumanne, Joho
aliwaambia wanahabari kwamba anajivunia alama ya mtihani ya D- ambayo alipata
katika mtihani wa kitaifa wa mwaka 1993.
Chanzo: BBC
No comments