Rubani afariki ndege ikiwa safarini
![Rubani afariki ndege ikiwa safarini Marekani](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/B476/production/_95389164_tv038721604.jpg)
NEW MEXICO,
Marekani
RUBANI wa
ndege aina ya Boeing 737-800 mali ya kampuni ya American Airlines, William ‘Mike’
Grubbs amefariki dunia ghafla wakati ndege hiyo ikiwa kilometa chache kutua
katika uwanja wa ndege wa Albuquerque.
Taarifa iliyotolewa
na shirika hilo, ilieleza kuwa rubani huyo alifariki wakati ndege hiyo ilipokuwa
ikielekea kutua katika uwanja huo wa Albuquerque kutoka ilikotokea Dallas.
Ndege hiyo
aina ya Boeng 737-800, ilikuwa umbali wa kilometa tatu kabla ya kutua, wakati
nahodha alipotangaza suala la dharura, kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege
wa Albuquerque
Ndege hiyo
ilitua bila ya kisa chochote na hakuna aliyejeruhiwa. Mwaka 2015, rubani
mwingine wa shirika hilo alifariki wakati wa safari kutoka Phoenix kuelekea
Boston.
Ndege hiyo
ilipelekwa na rubani mwenza kwa njia iliyo salama hadi uwanja wa Syracuse mjini
New York. BBC
No comments