Mo Dewji aitembelea Juventus na kuahidi kuiunganisha na Simba SC
Ofisa Mtendaji Mkuu
wa kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (METL), Mohamed Dewji ‘Mo’ akiwa
katika makao makuu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’,
Juventus FC alipotembelea hivi karibuni.
BILIONEA mwenye umri mdogo na mshindi
wa tuzo ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ amefanya ziara katika
makao makuu ya klabu ya mpira ya Juventus ya Italia na kuahidi kuwa atafanya
kila awezalo kuiunganisha na Simba SC ya Tanzania.
Juventus ambao ndiyo mabingwa watetezi
wa Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Serie A, imekuwa ikifanya vema katika misimu
ya hivi karibuni katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu Uefa
Champions League.
“Wiki hii nimekutana na Juventus FC,
ambayo ni klabu yenye mafanikio zaidi Italia licha ya kuwepo kwa klabu
nyinginezo kama vile AC Milan na Inter Milan”
“Ninatarajia kuitambulisha/kuiunganisha
timu hiyo kwa uongozi wa Simba ili kujadili mambo kadhaa ya hapa na pale. Pia wameahidi
kusaidia soka la Tanzania kwa kuendeleza soka la vijana” alisema Mo Dewji.
Chanzo: Azania Post
No comments