Dangote aapa kumtimua Wenger akiinunua Arsenal
LONDON- BILIONEA
namba moja Afrika, Aliko Dangote amesema ndoto yake ya kuinunua Arsenal bado
ipo na iwapo ataifanikisha, jambo la kwanza kulifanya klabuni hapo ni kumtimua
kocha Arsene Wenger.
Dangote
ambaye ni shabiki mkubwa wa timu hiyo, hakuwahi kuficha matakwa yake ya
kuinunua klabu hiyo licha ya kuwa mmiliki Stan Kroenke kusisitiza hana mipango
ya kuiuza.
Akizungumza na
Bloomburg, Dangote alisema kwamba; “Kitu cha kwanza kukifanya nikishainunua
Arsenal ni kubadilisha kocha. (Wenger) Amefanya kazi nzuri, lakini itakuwa
nafasi nzuri kwa kocha mwingine kujaribu bahati yake.”
Dangote
mwenye umri wa miaka 60, amesema kwa sasa ataendelea kupigania kuinunua timu
hiyo baada ya kukamilisha ujenzi wa mtambo wa kusafisha mafuta wenye thamani ya
pauni bilioni 8.5 (sh trilioni 24.6) Lagos nchini Nigeria.
Bilionea huyo
mwenye utajiri wa pauni bilioni 10 (sh trilioni 29) kwa sasa, anadai kuwa
Kroenke anayemiliki hisa asilimia 67 na Alisher Usmanov mwenye asilimia 30 ya
hisa za Arsenal, endapo watapewa dau zuri basi watashawishika kuuza klabu hiyo.
“Wakipata
dau lenye thamani kubwa, basi watashawishika kuiuza timu hiyo. Nitakapokamilisha
ujenzi wa mtambo huo, nafikiri nitakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya hivyo,”
alisema Dangote.
Tofauti na
matakwa ya Dangote kumtimua Wenger, kwa upande wake Kroenke anadai hana mpango
wa kuiuza timu hiyo na anamuunga mkono kocha huyo na amemsisitiza kuipa
mafanikio zaidi.
Daily Mail.
No comments