Header Ads

Qatar yaongezewa muda wa kutekeleza masharti



Map
RIYADH- SAUDI ARABIA na nchi tatu za kiarabu zimeongeza muda kwa Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.

Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika jana. Taifa hilo la Ghuba, linasema kuwa litajibu kupitia barua ambayo itawasilishwa kwa Kuwait leo Jumatatu.
Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani atasafiri kuenda Kuwait leo, kuwasilisha barua hiyo iliyotumwa kutoka kwa emir wa Qatar kwenda kwa emir wa kuwait ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa mzozo huo.
Siku ya Jumamosi, Sheikh Jassim Al-Thani, alisema kuwa taifa hilo lilikataa masharti hayo lakini liko tayari kwa mazungumzo.
Qatar imekuwa chini na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa wiki kadhaa sasa, kutoka Saudi Arabia, Misri, Falme za nchi za Kiarabu (UAE) na Bahrain.


No comments

Powered by Blogger.