Mugabe amzawadia shemejiye zawadi ya dola 60,000
HARARE- RAIS
Robert Mugabe amempa shemeji yake zawadi ya dola 60,000 (sh milioni 132) wakati
wa siku yake ya kuzaliwa, kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald.
Alisema kuwa,
zawadi hiyo ni ya kumshukuru shemejiye huyo, Junior Gumbochuma ambaye ni dada mkubwa
wa mke wake, Grace Mugabe, kwa kusaidia kuwalea watoto wa kiongozi huyo mkongwe.
Kupitia zawadi
hiyo kwa Gumbochumba ambaye ni mhubiri, Rais Mugabe alitumia fursa hiyo
kuwakosoa wahubiri wengine wa Pentecostal ambao hupata fedha kutoka kwa waumini
kwa kubuni miujiza ya uwongo.
BBC
No comments