Mourinho ataka kukaa Man United miaka 15

LOS ANGELES- KOCHA Jose Mourinho anataka kufuata nyayo za Sir Alex Ferguson katika
timu ya Manchester United kwa kuinoa kwa miaka mingi.
Akizungumza katika kambi ya maandalizi ya timu
yake kwa msimu mpya kwenye Uwanja wa UCLA nchini Marekani, Mourinho alisema
juzi anataka kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kwa miaka 15.
Mourinho (54) anainoa United kwa msimu wa pili
huku akiwa hajafanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi amesema anataka
kuinoa United kwa miaka mingi kama Ferguson kisha kustaafu.
“Niko tayari kwa hili. Ningependa kusema niko
tayari kwa miaka 15. Hapa? Ndiyo kwa nini isiwe hivyo? Ninakiri inaweza kuwa
ngumu sana kwa sababu ya presha inayozunguka kazi yetu,”
“Kila mtu amekuwa akiweka presha kwa makocha
na watu wakisema tunatakiwa kushinda, lakini kwa kweli mmoja kuweza kushinda
kila mwaka inakuwa ngumu sana,'' alisema.
No comments