Mata kuikosa Man City Marekani

LOS ANGELES-
KIUNGO wa Manchester United, Juan Mata,
anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja baada ya kuumia kwenye
mchezo wa kirafiki kati ya timu hiyo na Real Salt ya Marekani.
Mchezaji huyo alichezewa vibaya na Sebastian Saucedo, ambaye naye alikuja
kuchezewa vibaya na Antonio Valencia ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Katika mchezo huo, mchezaji mwingine wa Man United, Matteo Darmian
aliumia.
“Mata amepata jeraha la enka, ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa siku
kadhaa wakati Darmian hajapata tatizo kubwa,” alisema kocha wa Man United, Jose
Mourinho.
No comments