Lissu kupandishwa kizimbani leo
DAR
ES SALAAM- MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu,
leo atapandishwa tena kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini hapa,
kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili.
Lissu
ambaye alikamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita, anakabiliwa na kesi hiyo ambayo
ilianza kusikilizwa Jumatatu na kuahirishwa hadi leo huku wakili wake, Fatma
Karume, akiwa na imani kuwa mteja wake atapewa dhamana.
Fatma
amesema endapo Mahakama hiyo haitatoa dhamana kwa Lissu, watakata rufaa
Makahama ya Rufaa.
Lissu
anayetetewa na mawakili 18, anatuhumiwa kuwa Julai 17, akiwa mtaa wa Ufipa,
Kinondoni alitoa lugha ya uchochezi hali ambayo ingesababisha chuki kwa sababu
aligusa udini, ukabila na ukanda.
Julai
24, Mbunge huyo alinyimwa dhamana na kutakiwa abaki rumande hadi leo ambapo
Mahakama itatoa uamuzi wa dhamana, kutokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha
pingamizi.
Mahakama
hiyo ilifikia uamuzi huo, baada ya mawakili wa Lissu, Fatma na wa Serikali,
Mutalemwa Kishenyi na Saimon Wankyo kujibizana kwa hoja kwa zaidi ya saa mbili.
Baada
ya majibizano hayo, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi leo
ili apitie hoja hizo na kuziandikia uamuzi.
No comments