Kenyatta aionya mahakama Kenya
NAIROBI- RAIS
wa Kenya Uhuru Kenyatta ameionya idara ya mahakama nchini, akiitaka kutousaidia
upinzani na kuhujumu uchaguzi ujao.
Hayo yanajiri
baada ya Mahakama Kuu nchini, kutoa uamuzi mgumu wa kusimamisha zabuni ya
uchapishaji wa karatasi za kupigia kura iliyotolewa kwa kampuni ya Al Ghurair
ya Dubai, kwa madai kuwa ina uhusiano na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.
Kenyatta
alisisitiza kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa na kuongeza kuwa,
mahakama haiwezi kudai kuwa huru na kutumia uhuru huo kuingilia idara zingine
za Serikali.
Muungano wa
upinzani wa NASA ulidai kuwa, rais alikuwa na uhusiano na kampuni ya Dubai la
Al Ghurair ambayo ilishinda zabuni ya dola milioni 24 kuchapisha makatasi hayo.
Hata hivyo Jaji
Mkuu nchini, David Maraga, amemuonya Rais Uhuru Kenyatta kutohujumu imani ya
umma juu ya mfumo wa kisheria.
Nayo tume ya
Uchaguzi nchini (IEBC) leo inatarajiwa kukutana na wagombea wote wanane wa kiti
cha uraisi akiwemo Rais Uhuru Kenyata.
Mawakili wa IEBC
hiyo pia watafika mbele ya Mahakama ya Rufaa kupata ufafanuzi zaidi juu ya
uamuzi huo.
BBC
No comments