Jeshi la Iraq laukomboa mji wa Mosul

BAGHDAD- WAZIRI
Mkuu, Haider al-Abadi (pichani) ametembelea mji wa Mosul na kuwapongeza wanajeshi katika
kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu
(IS).
Hata hivyo,
hakutangaza rasmi ushindi, akisema hilo litafanyika pindi vikundi vilivyobaki
vitakapoondolewa. Mosul ndiyo sehemu ambayo kundi la IS lilipotangaza kuunda
uongozi wake miaka mitatu iliyopita.
Sehemu kubwa
ya mji huo imekuwa vifusi baada ya mapigano ya miezi tisa ya kuwaondoa
wapiganaji hao.
Abadi ametembea
katika barabara za mji wa Mosul na kuwapongeza wanajeshi. Wakati huo huo, kumekuwa na sherehe pindi
alipozuru eneo hilo.
Awali
kulikuwa na taarifa za kuwepo mapigano, na moshi mzito ukionekana juu ya eneo
ambao limekuwa ndio kitovu cha wapiganaji wa IS.
Kundi hilo
la IS, bado linahodhi sehemu ya Magharibi na Kusini mwa Mosul na inaaminika
litaendelea kufanya mashambulizi katika sehemu kubwa ya Iraq.
Islamic State
waliuteka mji wa Mosul mnamo June 2014 na kuanzisha utawala wao. Vikosi vya
Iraq, vikisaidiwa na mashambulizi ya anga kutoka Marekani, vimekuwa vikipambana
kuirudisha Mosul tangu Oktoba 17 mwaka jana.
Maelfu ya
raia wamekimbia huku wengine wakikosa pa kukimbilia wakati mapigano
yakiendelea.
BBC
No comments