Header Ads

Conte aongezewa miaka miwili Chelsea



Chelsea

LONDON- MENEJA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuwanoa mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya England.
Conte katika msimu wake wa kwanza, ameisadia Chelsea kutwaa ubingwa wa England kwa kushinda michezo 30, na kucheza fainali ya michuano ya kombe la FA ambayo walifungwa na Arsenal.
Baada ya kusaini mkataba huo mpya, Conte alisema; “Nimefurahi sana kusaini mkataba huu mpya. Natumaini tutaendelea kufanya vizuri kwenye mashindano yote.”
Naye mkurugenzi wa klabu hiyo, Marina Granovskaia, aliongeza kwa kusema; “Mafanikio makubwa waliyopata, pamoja na uhodari wa kocha huyo ndiyo kimewapa imani ya kumuongezea Conte mkataba mpya.”

No comments

Powered by Blogger.