Watu 22 wafariki ajali ya basi India

UTTAR
PRADESH, India
TAKRIBAN
watu 22 wamefariki dunia, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na
lori mjini hapa.
Ajali hiyo
ilitokea mapema leo, katika mji wa Bareilly uliopo kilometa 252 kutoka mji mkuu
wa jimbo, Lucknow.
Ofisa wa
cheo cha juu cha polisi mjini hapa, alisema waathiriwa wote kwenye ajali hiyo
walikuwa na majeraha mabaya na hawatambuliwa mara moja.
Basi hilo la
abiria lilishika moto kufuatia mgongano huo. Polisi wanamtafuta dereva wa lori
lililohusika kwenye ajali.
Shirika la
habari la AFP liliwanukuu polisi wakisema kuwa, milango ya basi iligoma kufunguka
baada ya mlipuko hali iliyosababisha abiria kukwama ndani ya basi.
Watu
wachache walifanakiwa kutoka nje kwa kuvunja madirisha ya basi.
India ina
viwango vya ju zaidi vya ajali za barabarani duniani, ambapo ajali hutokea
baada ya kila dakika nne.
No comments