IS wakiri kuhusika na shambulio la London
LONDON,
Uingereza
KUNDI la
kigaidi la Islamic State (Dola la Kiislamu) limekiri kuhusika kutekeleza
shambulio la kigaidi lililosababisha watu saba na kujeruhi wengine 50 jijini
hapa mwishoni mwa wiki.
Shambulio hilo
lililotokea katika daraja la juu la London maarufu London Bridge, lilitokea
baada ya magaidi hao kuwagonga watu kabla ya kuanza kuwachoma visu wengine.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini, ilieleza kwamba watu watatu
ambao walikuwa miongoni mwa washambuliaji hao waliuawa eneo la tukio na wengine
wanaendelea kusakwa.
Aidha,
Polisi wamebainisha kuwa wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini hapa,
hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi
ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao 50 walijeruhiwa.
Wachunguzi
wanajaribu kubaini, ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na
kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada
wowote.
Watu
11 wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi Mashariki mwa London. Kundi la
Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo. Mwanamke mmoja raia wa
Canada aliyeuawa katika shambulio hilo, ametajwa katika vyombo vya habari.
Taarifa ya
familia yake imesema kuwa, alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa
na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake. Watu 21 waliojeruhiwa
katika shambulio hilo wako katika hali mahututi.
No comments